
Kocha Mkuu wa Young Africans Marcio Maximo
(kushoto) akiongea na waandishi wa habari juu ya mchezo wa kirafiki dhidi ya
Big Bullets kutoka Malawi siku ya jumapili, kulia ni Afisa Habari wa timu hiyo
Bw Baraka Kizuguto
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
TIMU ya
Young Africans itashuka dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya
jumapili kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu
ya Big Bullets FC (zamani Bata Bullets) inayoshiriki Ligi Kuu ya TNM nchini
Malawi.
Young Africans
ambayo imeshacheza michezo minne mpaka sasa ya kirafiki ukiwemo mmoja wa
kimataifa katikati ya wiki hii dhidi ya timu ya Thika United kutoka nchini
Kenya imeshinda michezo yote.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika mkutano na waandishi wa habari, kocha mkuu wa
Young Africans mbrazil Marcio Maximo amesema mchezo huo wa siku ya jumapili
utakua ni kipimo kizuri kwa vijana wake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom
wiki mbili zijazo.
"Mchezo
uliopita tuliocheza dhidi ya Thika United ulikua ni mchezo mzuri, tumepata
nafasi ya kuyaona mapungufu yetu na kama mnavyofaham wenzetu wako katika Ligi
inayondelea hivyo walicheza kitimu zaidi kuliko sisi na hata Big Bullets FC pia
namini kitakua ni kipimo kizuri kwetu " alisema Maximo".
Kuhusu
timu ilivyocheza Maximo amesema hapendi kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja, na
masula ya uchezaji hapendi kuyaongea kwa jamii, hiyvo yeye kama kocha
alishaongea na wachezaji na kuwaelezea mapungufu yaliyojitokea na kipi
wanapaswa kukifanya katika michezo inayofuata.
Aidha
Maximo aliongeza kuwa yeye kwa sasa hana kikosi cha kwanza, hana mchezaji
mwenye uhakika wa namba, kilichopo kwake ni kundi la wachezaji ambao wote wana
nafasi ya kucheza kulingana na mahitaji ya mchezo wenyewe.
Afisa
Habari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto amesema taratibu zote za mchezo
zimekamilika na timu ya Big Bullets FC kutoka nchini Malawi inatarajiwa
kuwasili kesho jijini Dar es salaam na kufanya mazoezi jioni katika Uwanja wa
Karume eneo la Ilala.
"Mchezo
wa jumapili tunatarajia utakua ni mchezo mzuri, ukizingatia timu ya Big Bullets
FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Malawi iiliyofikia
mzunguko wa 17 kwa tofauti ya pointi moja na vinara, na kocha Maximo
alipendekeza tupate timu tofauti kutoka ukanda wa Kusini mwa Afrika baada ya
kuwa tayari tumeshacheza na timu ya Ukanda wa Afrika Mashariki" alisema
Kizuguto.
Siku ya
jumapili mechi inatarijiwa kuanza majira ya saa 10 kwa saa za Afrika Mashariki
na viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo:
VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/=
Orange Tshs 10,000/=
Blue & Green Tshs
5,000/=

0 comments:
Post a Comment