
Na Baraka Mpenja
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya
leo inachuana na Burundi mjini Bujumbura katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki
uliopo katika kalenda ya FIFA.
Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij inaingia
uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-0 na Burundi katika mechi
maalumu ya kirafiki kuadhimisha miaka 50 ya Muungano, Aprili 26 mwaka huu
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hata hivyo kikosi kilichocheza katika mechi hiyo
kilisheheni wachezaji waliotokea katika mpango maalumu wa TFF wa maboresho ya
Taifa Stars ambapo wachezaji wengi hawapo isipokuwa Joram Mgeveke wa Simba.
Nahodha wa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema
timu imeandaliwa vizuri na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.
Kuhusu wachezaji wawili hatari wa Burundi
wanaokipiga ligi kuu Tanzania bara, Amiss Tambwe (Simba) na Didier Kavumbagu (Azam
fc) Cannavaro alisema ni wachezaji wa kawaida na wameshawazoea, hivyo hawawezi
kuwapa shida.
“Ni wachezaji wa kawaida tu, tunakutana nao kila
siku, nadhani tutapambana vizuri na tutapata ushindi”. Alisema Cannavaro.
“Hata sisi tunawafahamu Amiss (Tambwe) na Didier (Kavumbagu).
“Tunawafahamu udhaifu wao na wao wanatufahamu,
hata mimi naweza kufunga kutokana na ujuzi wangu”.
“Hata tulipokwenda Msumbiji tulicheza vizuri na
tulipata goli, lakini hatakufanikiwa kusonga”. Alisema Cannavaro.
Kila la heri Taifa stars katika mchezo wa leo.
0 comments:
Post a Comment