
Samir Nasri haoni kama Liverpool wataitishia Manchester katika mbio za ubingwa msimu huu.
SAMIR Nasri anadai Chelsea na Manchester United zitaitishia zaidi Manchester City msimu huu, lakini Liverpool wana mlima mzito wa kuwania ubingwa.
Kikosi cha Brendan Rodgers kilikosa ubingwa kwa tofauti ya pointi mbili tu na mabingwa Man City, lakini kiungo huyo wa Ufaransa anaamini kwamba kitendo cha wekundu hao wa Anfield kushiriki ligi ya mabingwa kutawapa changamoto zaidi.
"Liverpool watakuwa na wakati mgumu zaidi kwasababu wamempoteza Luis Suarez na watacheza ligi ya mabingwa, kwahiyo itakuwa tofauti kwao" . Amesema Nasri.

Furaha ya Cesc:Kuwasili kwa mchezaji mwenzake wa zamani na Nasri, Cesc Fabregas kumeipa nguvu zaidi Chelsea
0 comments:
Post a Comment