Saturday, September 6, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MZAMBIA Patrick Phiri anatarajia kuiongoza Simba sc katika mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya itakayopigwa leo jioni uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kivutio kikubwa katika mechi ya leo ni mshambuliaji wa Simba aliyesaini mkataba wa miezi sita kuitumikia klabu hiyo akitokea kwa mahasimu wao Yanga sc, Mganda Emmanuel Anord Okwi.

Ingawa usajili wake una utata kwasababu uongozi wa Yanga chini ya mwenyekiti wake, Yusuf Manji unadai una mkataba na Okwi, Simba wanatarajia kumtumia nyota huyo wakiamini wako sahihi kumsainisha.

Kesi ya Okwi ipo Shirikisho la soka Tanzania TFF na kinachosubiriwa ni tamko tu ili kujua Mganda huyo mwenye kasi uwanjani na chenga za maudhi atakipiga wapi, Simba au Yanga.

Katika mazoezi ya Simba yaliyokuwa yakiendelea uwanja wa Uninio, Bunju, jijini Dar es salaam, Okwi alikuwa kivutio kwa mashabiki waliohudhuria kuona wachezaji wao.


Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange 'Kaburu' (kushoto) akiwa na Okwi

Okwi alionekana kuwa na kasi uwanjani, alimiliki mpira, alikuwa anapiga chenga zake za maudhi na kusonga mbele.

Mara kadhaa mashabiki walikuwa wanampigia makofi mazoezi kuashiria kukubali kwa kile anachofanya.

Baada ya mechi ya leo, kikosi cha Patrick Phiri kitarejea Zanzibar kuendelea kumalizia program zake za maandalizi kabla ya ligi kuanza septemba 20 mwaka huu.

Awali Simba walipanga kuchuana na Mtibwa Sugar, lakini kocha Phiri akapendekeza kutafutiwa mechi ngumu ya kimataifa ili kuangalia namna kikosi chake kilivyoimarika.

Viingilio katika mechi hiyo ni shilingi elfu 5 (5,000) kwa viti vya kijana, viti vya rangi ya chungwa ni shilingi 10,000, VIP C na B itakuwa shilingi 2,000 wakati VIP A itakuwa shilingi elfu 30,000.

Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa leo kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi.


Simba wataanza kampeni za kusaka ubingwa wa ligi kuu bara septemba 21 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Coastal Union.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video