
Na
Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Ili
kujiimarisha zaidi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara, klabu ya
Mbeya City inataraji kucheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki kabla ya
kuanza kwa msimu mpya Septemba 20 ambapo timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya
tatu msimu uliopita itafungua dimba dhidi ya ' Maafande' wa JKT Ruvu katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kocha
mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi ameuagiza uongozi wa timu hiyo kumtafutia
michezo miwili dhidi ya klabu za Malawi.
Big
Bullets ni klabu kongwe nchini Malawi na Kusini mwa bara la Afrika itacheza na
City katika mchezo wa kwanza wa kimataifa.
" Nimeuambia uongozi wangu nahitaji mechi
mbili ngumu za kimataifa na timu kutoka nchini Malawi. Tunataraji kucheza na
Big Bullets ya Malawi ili kujiimarisha zaidi kabla ya kuanza kwa msimu
mpya" alisema, Mwambusi.
City
imefanikiwa kuwabakisha kikosini wachezaji wake nyota kama, Paul Nongwa, Saad
Kipanga, Hassan Mwasapili, na golikipa, David Baruani licha ya wachezaji hao
kuwaniwa na timu kubwa katika dirisha la usajili.
Mwagane
Yeya, Eric Banda wataungana na nyota mpya, Themi Felix kuifanya timu hiyo
kuendelea kuwa bora katika msimu wake wa pili katika ligi ya Tanzania Bara.

0 comments:
Post a Comment