Muda wa maajabu: Kiungo wa Watford akifunga bao la kusawazisha
MFUNGAJI wa goli la Scotland katika kipigo cha 2-1 kutoka kwa Ujerumani jana usiku, Ikechi Anya alishangilia bao hilo huku akidai haamini kama kweli ametia mpira kambani.
Anya alifunga bao hilo katika dakika ya 66 kusawazisha lile la Ujerumani lililofungwa na Thomas Muller, ingawa mshambuliaji huyo wa Bayern Munich aliongeza bao la pili dakika nne baadaye.
Mshambuliaji huyo wa Watford, Anya, kupitia mtandao wa kijamii aliwashukuru mashabiki waliosafiri kuhudhuria mechi hiyo na kueleza kuwa hakuamini kama alimfunga Manuel Neuer, ambaye ni kipa bora duniani.

Furaha: Anya aliandika katika mtandao wa Twita akielezea furaha yake ya kuifungia goli nchi yake

0 comments:
Post a Comment