
Karudi Palace: Andrew Johnson amesaini mkataba mfupi na kujiunga tena na Eagles.
CRYSTAL Palace imeongeza mchezaji mwingine kwa kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani, aliyesaini mkataba mfupi akiwa huru, Andrew Johnson.
Nyota huyo mwenye miaka 33 amesaini mkataba atakaomfanya acheze katika klabu hiyo ya kusini mwa London mpaka mwezi januari.
Johnson, ambaye aliichezea Everton, Fulham na Queens Park Ranger ,aliondoka Selhurst Park mwaka 2006.

Kipenzi cha mashabiki: Mmiliki wa zamani wa Crystal Palace ,Simon Jordan alimsajjili Johnson klabuni hapo mwaka 2002

Gwiji: Johnson ni mtu wa kuabudiwa katika dimba la Selhurst Park kwasababu ya rekodi yake ya ufungaji wa mabao
Johnson alijiunga na Palace kutokea Birmingham mwaka 2002 na alikuwa kipenzi cha mashabiki baada ya kuisaidia klabu hiyo kupanda ligi kuu mwaka 2004.
Alifunga mabao 21 msimu uliofuata na kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha England, lakini alishindwa kuizuia Palace kushuka daraja.
Johnson, akizungumza na tovuti ya Crystal Palace alisema: "Nimefurahi kurudi tena katika klabu ninayoipenda zaidi".
0 comments:
Post a Comment