
Enzi za furaha: David Beckham akishangilia baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Ugiriki mwaka 2001 na kuiwezesha England kufuzu fainali za kombe la dunia katika uwanja wa Old Trafford
DAVID Beckham bado mpira wa miguu uko kwenye damu yake na mapenzi aliyonayo katika mchezo huo maarufu duniani yanamfanya akose raha ya kukaa bila kucheza.
"Nakumbuka kuichezea England kuliko kitu chochote," amekiri wazi.
Timu ya England ilipocheza mechi ya kirafiki na Norway katika dimba la Wemley mbele ya mashabiki 40,000 inaonekana kuwa jambo jema katika moyo wa Beckham.
Ni miaka mitano sasa tangu Beckham astaafu kuvaa jezi ya England baada ya kuichezea mechi 115 na hatimaye kutandika daluga katika mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Belarus ndani ya uwanja wa Wembley.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United aliifungia England mabao 17.
Kwa mtu wa mpira Beckham ambaye alikuwa tunu ya soka duniani kote, jezi nyeupe bado ina maana kubwa kwake.

Kocha? Beckham akiwa benchi katika fainali za kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika kusini ambapo England ilijeruhiwa pia.
Beckham alisema: "Bado napenda kukaa na wenzangu, napenda mechi, napenda nilivyokuwa nahodha kwa mechi 59, napenda kila kitu kuhusu England".
"Kuna mambo mengi ya kujivunia kama mchezaji. Naikumbuka Manchester United na Real Madrid na timu nyingine zote nilizocheza, lakini nakumbuka kuichezea England kuliko kitu chochote kile"

0 comments:
Post a Comment