Thursday, September 11, 2014

Kocha mkuu wa Misri, Shawky Gharib

MWENYEKITI wa chama cha soka cha Misri, Gamal Allam amemhakikishia kocha mkuu wa timu ya Taifa ya nchi hiyo, Shawky Gharib kwamba hatafukuzwa.

Mafarao walipoteza mechi ya pili ya kufuzu AFCON 2015 baada ya kufungwa 10 na Tunisia na kupunguza matumaini ya kusonga mbele katika safari hiyo ya Morocco.

Misri walifungwa 2-0 katika mechi ya kwanza ya makundi dhidi ya Senegal.

“Shawky Gharib hataondoka katika nafasi yake, ataendelea kuwa kocha wa Mafarao,” Allam alisema baada ya mechi.

“Kwasasa siwezi kulizungumzia zaidi hilo, tutakuwa na kikao naye na benchi zima la ufundi kuzungumzia sababu za timu kupoteza mechi mbili.”

Mashabiki wa Misri waliohudhuria mechi hiyo walikitaka chama cha soka nchini humo kumfukuza kazi kocha mkuu.

Misri itacheza mechi nyingine dhidi ya Botswana mwezi Oktoba mwaka huu.


Mafarao hawajawahi kufuzu AFCON tangu walipotwaa ubingwa mwaka 2010 nchini Angola.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video