
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Agosti 7, 2014, saa 5:11 asubuhi
MAGWIJI wa Real Madrid maarufu kama ‘Real Madrid
Legends’ wanatarajia kufanya ziara nchini Tanzania kuanzia Agosti 22 mwaka huu
ambapo watacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya kikosi maalumu cha nyota wa
Tanzania Agosti 23 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kiingilio cha chini katika mechi hiyo ya
kihistoria kitakuwa buku tano tu (5,000)
na lengo ni kuwapa fursa Watanzania wengi kuwaona Magwiji wa Bernabeu waliowahi
kutamba katika michuano ya La Liga, UEFA na kombe la dunia wakiwa na nchi zao.
Kwa mujibu wa meneja wa ziara hiyo, Dennis Ssebo,
wachezaji mbalimbali wameshathibitisha kuwasili Tanzania na maandalizi kwa
ujumla yanakwenda barabara.
Mtandao huu kuanzia leo utakuwa unaangazia
historia fupi ya magwiji wote watakaokuja nchini, yaani kuanzia wa kwanza mpaka
wa mwisho na leo hii tunaanza na:

1.
PEDRO CONTRERAS GONZÁLEZ-
Huyu ni kipa mstaafu wa Hispania. Alizaliwa mwaka
Januari 7, 1972 mjini Madrid. Urefu wake ni futi 5 na inchi 11.
Kipa huyo alicheza mechi 246 za La Liga katika
misimu 13 aliyokaa langoni. Alizichezea klabu za Real Madrid, Rayo Vallecano,
Malaga na Betis na kumalizia soka lake katika klabu ya Cadiz CF, msimu wa
2007-08.
Katika fainali za kombe la dunia mwaka 2002 ambapo
Brazil chini ya kocha Luis Felipe Scolari walitwaa kombe nchini Korea kusini na
Japan, Contreras aliichezea timu yake ya taifa ya Hispania kwa mara ya kwanza na
ya mwisho.
Hili ni zao la Real Madrid katika mfumo wake wa
soka la vijana. Kipa huyu aliyezaliwa mjini Madrid, alivaa medali ya UEFA mwaka
1998, lakini hakucheza hata dakika moja katika msimu huo.
Alikaa miaka minne na kikosi B, Real Madrid Castilla
na alionekana katika michezo minne ya timu ya kwanza msimu wa 1998-99 ambapo
Real Madrid ilimaliza katika nafasi ya pili.
1996-97 alitolewa kwa mkopo kwenda klabu ya Rayo
Vallecano ambapo alikosa mechi moja tu ya ligi kuu katika mechi 42.
Contreras alijiunga na Malaga FC katika msimu wa
1999-2000. Alikuwa kipa chaguo la kwanza ambapo alikosa mechi sita tu kutoka
1999-2003.
Kipa huyo alijiunga na Real Betis mwaka 2003,
ambapo alicheza mechi 22 za ligi kuu katika msimu wa 2003-04, na nyingine
alizikosa baada ya kupata majeruhi na kumpisha Toni Doblas.
Msimu wa 2005-06 alishindani katika makombe ya
UEFA na ligi ya mabingwa ampapo hakufungwa bao katika mechi mbili dhidi ya
Chelsea katika ushindi wa 1-0 hatua ya makundi.
Alitolewa kwa mkopo Cadiz CF msimu wa 2007-08
akicheza sambamba na Dani. Contreras aliachwa baada ya msimu kumalizika. Baada
ya hapo alistaafu soka na kujiunga na klabu yake ya zamani ya Malaga kama kocha
wa makipa.
MAKOMBE ALIYOSHINDA
Real Madrid
Málaga
Betis
Kesho tutakuletea historia ya gwiji mwingine
atakayetua Tanzania, Agosti 22 mwaka huu, ni nani huyo? tafadhali endelea
kutufuatilia….
0 comments:
Post a Comment