Sunday, August 17, 2014


Wachezaji wa Coastal Union wakiwa mazoezini uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

Imechapishwa Agosti 17, 2014, saa 6:43 mchana

WAGOSI wa Kaya, Coastal Union wenye makazi yao jijini Tanga, ‘Waja leo waondoka leo’ wanaendelea kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.

Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mkenya, Yusuf Chipo amesema tatizo linalofanyiwa kazi kwasasa ni safu butu ya ushambuliaji, hivyo wanafanya usajili makini kuhakikisha wanaiboresha.

“Tatizo la Costal Union kwa siku nyingi ni safu ya ushambulizi na katika usajili wetu tumekuwa tukitilia mkazo sehemu hii ya mbele. Tunatafuta wachezaji wazuri wenye uzoefu, na nadhani kwasasa tumepata jawabu letu” Alisema Chipo.

“Baada ya kusajili. Kilichobaki sasa ni kuwafanyisha watu mazoezi ili waelewane, watu waingiane na tumalizie usajili”

Hata hivyo, Chipo alisema ili kujipanga zaidi wanahitaji kuweka kambi ya maandalizi kisiwani Pemba.

“Tuna mipango ya maandalizi, tunataka kucheza mechi za kirafiki. Kuna safari tunaandaa ya kwenda Pemba ambapo tutakaa kwa wiki tatu au nne kwa ajili ya maandalizi’. Alisema Chipo.

Coastal Union watakutana na Yanga sc ambao wanatarajia kuelekea Pemba wiki ijayo kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya ligi kuu bara.

Kocha mkuu wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo alipendekeza kambi kuwekwa Pemba ili kuwapa wachezaji wake mazoezi katika hali ya utulivu.

Wakati huo huo, Wekundu wa Msimbazi Simba wamejificha kisiwani Unguja wakijiwinda na msimu mpya wa ligi kuu.


Kocha mpya wa Simba sc, Mzambia, Patrick Phiri amesifu mazingira ya Zanzibar na kusema yatamfanya ajipange vizuri na kampeni za kuusaka ubingwa wa ligi kuu bara.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video