
RWANDA itakata rufaa
dhidi ya maamuzi ya kuwaondoa kushiriki hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya
kucheza fainali za mataifa ya Afrika baada ya kumtumia mchezaji asiyekuwa na
sifa.
Shirikisho la nchi
hiyo limethibitisha kuwa lipo tayari kukata rufaa na litaipeleka kesi hiyo
katika mahakama ya juu ya rufani ya michezo kama maamuzi hayo hayatafutwa.
Rwanda iliondolewa
katika mashindano jumamosi na kamati ya
mashindano ya shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Hatua hiyo inafuatia malalamiko kutoka kwa shirikisho la
soka la Jamhuri ya Congo kuwa Rwanda ilimtumia mchezaji Birori Dady ambaye hati
zake za kuzaliwa ni tofauti na zile zilizowasilishwa kabla ya mechi ya mchujo
wa kombe la mabingwa barani Afrika dhidi ya DRC mwezi uliopita huko
Pointe-Noir.
Shirikisho la Congo lilidai kuwa
mchezaji huyo, Birori Dady anayeichezea
AS Vita anatumia hati ya Congo yenye jina la Etekiama Agiti Tady.
CAF walizifanyia uchunguzi nyaraka
zilizotolewa na mashirikisho ya Rwanda, Congo na DR Congo na pia walimhoji
mchezaji Agosti 11 makao makuu ya CAF mjini Cairo, Misri.
Wakati Rwanda wanaendelea kushikilia
msimamo kuwa mchezaji Dady Birori ana
hati moja ya utambulisho wa uraia, uchunguzu unaonesha kuwa alitumia jina la
Etekiama Agiti Tady wakati wa kujiunga na timu ya taifa.

Mchezaji aliyeigharimu Rwanda
CAF alisimamia ukweli kwamba mchezaji
ana hati mbili zenye majina mawili na umri tofauti na kusema hati hizo zinamhusu
mtu mmoja.
Baada ya hapo, Shirikisho hilo
lilitangaza kumsimamisha mchezaji mpaka hapo watakapotoa taarifa zaidi na
kumfungia kuichezea klabu yake na timu ya taifa ya Rwanda.
Rwanda iliitoa Congo kwa mikwaju ya penalty
baada ya mechi mbili na kufuzu hatua ya makundi, lakini sasa timu iliyofungwa
ndio imefuzu kwenda kundi A la kuwania kufuzu fainali za AFCON nchini Morocco
2015 ambapo itakutana na Nigeria, Sudan Na Afrika kusini.
Hata hivyo CAF imesema itatoa maamuzi
zaidi kama itaongeza adhabu baada ya kikao cha kamati ya mashindano
kitakachofanyika Septemba 17 mwaka huu.
CAF imetoa wito kwa wachezaji na
wadau wa soka kuwa makini na uraia wa nchi mbili.

0 comments:
Post a Comment