Mambo dole: Pepe Reina amekamilisha vipimo vya afya Bayern Munic.
Imechapishwa Agosti 8, 2014, saa 2:09 asubuhi
PEPE Reina anasaini mkataba wa kuitumia klabu ya Bayern Munich leo ijumaa baada ya kufuzu vipimo vya Afya klabuni hapo.
Mlinda
mlango huyo amefuzu vipimo vya afya katika uwanja wa mazoezi wa klabu
hiyo baada ya Liverpool kukubali kumuuza Mhispania huyo kwa paundi
milioni 20.
Reina amekosa mvuto katika miaka ya karibuni Anfield na msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya Napoli.
Bayern Munich walitweet jana usiku kuwa: Karibu Munich @PReina25! vipimo vya afya vimefanikiwa, mkataba utasainiwa kesho (leo).
Reina alikuwa kipa namba moja wa Liverpool baada ya kuwasili kutokea Villarreal mwaka 2006, na kucheza fainali ya UEFA.
Lakini baada ya Brendan Rodgers kumleta kipa wa Sunderland msimu uliopita, nafasi yake ilipotea.

0 comments:
Post a Comment