
Walizinguana: Argentina Sergio Aguero na Marcos Rojo walitamkiana maneno makali katika fainali za kombe la dunia.
MECHI ya watani wa jadi nchini England baina ya Manchester United na Manchester City "The Manchester derby" itakuwa na ladha tofauti msimu huu ambapo nyota wawili wanaocheza timu ya taifa ya Argentina, Sergio Aguero na Marcos Rojo watakutana.
Wachezaji hao wawili waliocheza fainali ya kombe la dunia walisemekana kutamkiana maneno makali wakati wa mashindano ya majira ya kiangazi nchini Brazil baada ya Rojo ambaye amekamilisha kujiunga na Manchester United kwa paundi milioni 16 kutoka klabu ya Sporting Lisbon kumkaribisha rafiki yake, mkali wa muziki wa Pop nchini Argentina, El Polaco ndani ya chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo wa makundi.
Kwa bahati mbaya, El Polaco alikuwa mpenzi wa zamani wa demu wa sasa wa Aguero, mwanamuziki mwingine wa Pop wa Argentina, Karina Tejeda.

Shangwe: Rojo alikuwa miongoni mwa nyota walioifikisha fainali Argentina

Wapenzi: Sergio Aguero akiwa na mpenzi wake Karina La Princesita kwenye mtandao wake rasmi wa Twita.
Waimbaji hao nyota wanaoimba muziki wa Cumbia, staili maarufu ya Latin, wana mtoto wa kike mwenye miaka minne, lakini waliachana mwaka uliopita na Aguero kujibebea 'Totoz'.
Kwa mujibu wa gazeto La Gaceta, Aguero hakufurahishwa na kitendo cha Rojo kumkaribisha mwanamuziki huyo katika chumba cha kubadilishia nguo ikizingatiwa jamaa alikuwa 'anapiga demu' wake hapo nyuma, yaani wamepita sehemu moja, si mchezo aisee!.
Aguero na Rojo walionekana kumaliza tofauti zao kwenye mechi zote zilizosalia za kombe la dunia, huku wawili hao wakicheza mechi ya nusu fainali na fainali baada ya Aguero kupoma majeruhi yake.
Lakini wanaweza kuzua jambo wakati wa kushikana mikono kwenye mechi ya mahasimu wa Manchester watakapokutana novemba 2 mwaka huu.
Kama sehemu ya dili lililomfanya Rojo ajiunge Old Trafford, Nani amerudi Sporting, ingawa United watamlipa nyota huyo mwenye miaka 27 mshahara wa paundi milioni 4.8 katika kipindi chote cha mkataba wa mkopo wa muda mrefu.

Nyota wawili: Princesita, mwanamuzi maarufu wa muziki wa Pop nchini Argentina, ndiye chanzo cha tatizo kwa wachezaji hao wawili

Dole: Siku za nyuma demu wa Aguero alikuwa mpenzi wa El Polaco, nyota mwingine wa Pop na rafiki mkubwa wa Rojo.
0 comments:
Post a Comment