Friday, August 15, 2014

Na Mwandishi Wetu, Tanga

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umeizidi kete klabu ya
Simba SC baada ya kumsajili kiungo kati wa timu ya Gormahia ya nchini
Kenya,Rama Saluma Mohamed aliyekuwa akiwaniwa na klabu hiyo.

Rama ametua kwenye klabu ya Coastal Union  akitokea nchini Kenya
na kusaini  mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha mwaka
mmoja.

Rama aliyewahi kuicheza timu hiyo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa
kupata namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harembee Stars
alitua jijini Tanga juzi usiku akiwa na kulakiwa na viongozi wa klabu
hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya Klabu
hiyo barabara 11,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema kikosi cha cha timu hiyo msimu ujao kinatarajiwa kuwa tishio kutokana na kufanya usajili wa nguvu ambao unaonekana utaleta upinzani mkubwa sana.

Aidha amesema kikosi chetu msimu ujao kitakuwa tishio kwa
sababu tunamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na usajili imara ambao tumeufanya kwa kusajlili wachezaji nyota kama vile Obina,Shabani Kado Sued Tumba ,Bakari Mtama, na wengine wengi walipo kwenye kikosi cha timu hiyo

Amesema bado wanaendelea na mchakato wa kuhakikisha wanaimarisha kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.


0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video