Imechapishwa Agosti 15, 2014, saa 11:53 jioni
KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone anaamini
timu yake ina safu kali ya ushambuliaji na kusema hana mpango wa kumsajili
mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres.
Mabingwa hao wa Hispania walimpoteza Diego Costa
na David Villa katika safu yao ya ushambulaiji majira ya kiangazi mwaka huu,
lakini wamefanikiwa kumsajili Mario Mandzukic, Antoine Griezmann na Raul
Jimenez katika wiki za karibuni.
Kwa usajili huyo, Muargentina huyo anahisi safu ya
ushambuliaji imekamilika , hivyo hana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea.
“Nadhani unapokuwa kocha na hauna uwezo mkubwa wa
kiuchumi lazima uendane na mazingira,” aliwaambia La Sexta.
“Nina furaha. Nadhani baada ya kumsajili Jimenez
tumepata kile tunachokihitaji kama timu”.
“Nadhani kuwa na Antoine Griezmann, Raul Garcia,
Mario Mandzukic na Jimenez inamaanisha tuna nguvu ya kutosha”.


0 comments:
Post a Comment