Imechapishwa Agosti 15, 2014, saa 11:57 jioni
WINGA wa Bayern Munich, Arjen Robben ameweka wazi
kuwa bado hajawa fiti kucheza akitokea katika mapumziko, baada ya kumaliza kucheza fainali za kombe la
dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil akiwa na timu ya taifa ya
Uholanzi.
Mholanzi huyo alikuwa miongoni mwa nyota wa Louis
van Gaal waliofika hatua ya nusu fainali katika mashindano hayo na kutolewa kwa
mikwaju ya penalty na Argentina.
Robben mwenye miaka 30 aliikosa mechi ya
DFL-Supercup dhidi ya Borussia Dortmund na anahisi anahitaji kujifua zaidi ili
kujiimarisha na kuanza kuiwakilisha Bayern.
“Ndivyo tulivyokubaliana kwasababu mechi ilikuwa
karibu sana,” aliiambia tovuti rasmi ya klabu alipoulizwa kutokuwepo katika
mechi hiyo.
“Nahitaji kufanya mazoezi ya nguvu kwa siku chache
na kurudisha kasi yangu. Bado nipo katika maandalizi ya kabla ya msimu. Hamu ya
kucheza mpira bado haijaja. Nipo tayari kuanza upya”.


0 comments:
Post a Comment