Na Mwandishi Wetu, Tanga
Imechapishwa Agosti 5, 2014, saa 7:00 mchana
TIMU ya Coastal Union ya Tanga inatarajia kucheza mechi mbili za
kirafiki katikati ya wiki hii ambazo zitachezwa kwa nyakati tofauti ikiwa ni
maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajiwa
kuanza mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza jana, Meneja wa timu ya Coastal Union, Akida Machai
alisema mechi hizo zitachezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga ambapo ya
kwanza itachezwa Kesho(leo) kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
Machai alisema mechi hiyo itakuwa dhidi ya Muheza Shooting na
maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa asilimia mia moja na
kinachosubiriwa ni siku ya mechi hiyo.
Alisema mechi ya pili itachezwa Ijumaa wiki hii dhidi ya AFC ya
Arusha kwenye uwanja wa Mkwakwani lengo likiwa kukipa makali kikosi hicho cha
ligi kuu soka Tanzania bara.
“Kama nilivyosema mechi hizi zote ni
muhimu sana kwa kila timu ambapo baada ya kumalizika uongozi utaangalia ni timu
gani ya kwenda kucheza nayo “Alisema Machai.
Hata hivyo aliwataka wapenzi na wanachama kujitokeza kwa wingi
kushuhudia mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.
0 comments:
Post a Comment