Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU
ya Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kuondoka mkoani Tanga kesho
kuelekea Visiwani Pemba kwa kutumia usafiri wa
Ndege kwa ajili ya kuweka
kambi ya Mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania
bara itakayoanza Septemba 20 mwaka huu.
Ofisa
Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa timu hiyo itaondoka
kesho saa tatu asubuhi kwenye uwanja wa Ndege jijini Tanga wakiwa
na msafara wa wachezaji 28 na viongozi sita.
Assenga
amesema kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kufanya mazoezi yake kwenye
viwanja vya Migombani visiwani humo asubuhi na jioni wakiwa na lengo
kuu la kuhakikisha wanajiandaa vema na michuano ya Ligi kuu soka Tanzania
bara.
Amesema
kuwa kati benchi la ufundi litakuwa likiongozwa na Kocha Mkuu wa
timu hiyo Yusuph Chippo, Msaidizi wake Benard Mwalala, Kocha wa Makipa
Razack Siwa na daktari wa timu na mtunza vifaa.

0 comments:
Post a Comment