
Maujanja: Alex Oxlade-Chamberlain akionesha uwezo wake wa kupiga 'drums' mpya aliyozawadiwa.
ALEX Oxlade-Chamberlain haridhiki kuonesha vipaji vyake nje ya kucheza soka katika klabu ya Asernal.
Japokuwa kipaji cha soka ndio kinamuweka mjini, lakini amejaaliwa vipaji vingine.
Nyota huyo mwenye miaka 21 alionesha ujuzi wake wa kupiga 'Drums' katika video fupi aliyoposti katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Kakumbushia enzi zake: Nyota wa Asernal alikuwa anapiga drums tangu akiwa na miaka 13.
Aliposti video fupi katika mtandao wa kijamii akiwaambia mashabiki wake kuwa amepewa 'drums' mpya na mama yake.
Alisema: "Mama yangu alininunulia wakati wa siku yangu ya kuzaliwa".
"Kwa mara ya kwanza nilipiga drum tangu nikiwa na miaka 13!! mtaalamu yeyoto wa Drums anaweza kunipa ujuzi zaidi?
Kiungo huyo mshambuliaji alitokea benchi katika suluhu ya bila kufungana baina ya Asernal dhidi ya Besiktas ligi ya mabingwa barani Ulaya siku ya jumanne.
Winga huyo anajiamini kuwa uwezo mkubwa wa kiufundi wa Asernal utawafanya waitoe Besiktas na kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.
0 comments:
Post a Comment