Maisha mapya: Alexis Sanchez akipozi katika picha akivalia jezi yake ya Asernal kama ishara ya kufungua ukurasa mpya wa maisha ya soka.
ARSENAL imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Barcelona, Alexis Sanchez - kwa dau la paundi milioni 30.
Kwa usajili huo, Asernal wanaamini nyota huyo ataweza kuwasaidia katika harakati zao za kutafuta ubingwa wa ligi kuu msimu ujao pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Nyota huyo wa Chile ambaye alikatisha likizo yake na kwenda London kukamilisha usajili, alifuzu vipimo vya afya na kukubali kusaini mkataba wa miaka minne-huku kukiwa na kipengele cha kuongeza miezi 12 na mshahara utakuwa paundi laki moja na elfu 40 kwa wiki.
Kiwango hicho kitamfanya alipwe sawa na kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo, Mjerumani, Mesut Ozil ambaye kwasasa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Emirates.
'Nina furaha sana ya kujiunga na Asernal, klabu yenye kocha mkubwa, kikosi bora cha wachezaji, sapoti kubwa duniani kote na uwanja mkubwa mjini London," alisema nyota huyo mwenye miaka 25.
Usajili mzuri: Kuna imani kuwa Asernal wanaweza kufanya makubwa msimu ujao baada ya kumsajili Sanchez.
Sanchez amejiunga na Asernal akitokea klabu ya Barcelona na amefurahishwa na sapoti ya mashabiki wa klabu yake mpya.
Anaangalia mbele: Sanchez ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Arsene Wenger majira haya ya kiangazi.

0 comments:
Post a Comment