Manchester United lazima waguse mfuko kama wanataka kumsajili nyota wa Ureno William Carvalho.
Manchester United imeambiwa kuwa inatatakiwa kulipa paundi milioni 37 kama inataka kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho.
Man United wamejaribu kuomba kupunguziwa bei wakati Chelsea nao wameonesha nia ya kutaka kumsajili, lakini klabu hiyo ya Ureno imeonya kuwa haitamuuza kwa bei rahisi.
Anazivutia klabu: Chelsea pia wameeleza kuvutiwa na nyota huyu wa Sporting.
Mkurugenzi wa michezo wa Sporting, Augusto Ignacio alisema: "Sio kama miaka ya nyuma wakati wachezaji wa Sporting walikuwa wanauzwa kwa bei yoyote. Kuvunja mkataba kunaihakikisha Sporting dili kubwa. Nimevutiwa na makubaliano".

0 comments:
Post a Comment