Hana bei: Rais wa Barcelona amesema Lionel Messi hauziki.
RAIS wa Barcelona imesisitiza kuwa Lionel Messi "hauziki" wakati huu miamba hiyo ya katalunya ikihangaika kumuongeza katika kikosi chao Luis Suarez msimu ujao.
Kwa sasa Messi anaichezea timu ya taifa ya Argentina katika fainali za kombe la dunia na ameshafunga mabao manne na kuifikisha hatua ya robo fainali.
Nyota huyo mwenye miaka 27 siku za karibuni alisaini mkataba na Barcelona ambao utamuingizia paundi milioni 16.3 kwa mwaka.
Rais wa klabu, Josep Maria Bartomeu alisema: "Nikiwa nahusika moja kwa moja, Messi hataki kuondoka. Tulimpa mkataba mpya siku si nyingi na ana furaha".
Kiungo wa Barca , Xavi (kulia) bado hajaamua hatima yake
Bartomeu pia alisema Xavi anaweza kuondoka klabuni hapo, lakini hajaamua bado ataelekea wapi.
"Xavi ana haki ya kuamua anataka kufanya nini na tutaheshimu suala hilo. Siku moja atarudi klabuni kwasababu ana uwezo wa kuwa kocha mkubwa".
Barcelona walishafungua ofa ya paundi milioni 72 siku ya jumatano usiku, lakini Liverpool wanata mkwanja wa paundi milioni 80 ili kumuuza nyota huyo mwenye miaka 27.
Enlarge
Messi akitaniana na mchezaji mwenzake wa Argentina Fernando Gago.

0 comments:
Post a Comment