
Mkenya, Tom Alex Olaba anaendelea na mkakati wake wa kusuka kikosi chake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi mwezi agosti mwaka huu.
Na Frank
Momanyi, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 2, 2014, saa 9:16 alasiri
BAADA ya kuingia kambini mapema kabisa, klabu ya wapiga kwata wa Ruvu Shooting yenye maskani yake mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani imeendelea kujiimarisha kwa kufanya usajili wa wachezaji wapya kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha mkuu, Mkenya, Tom Alex Olaba.
Afisa
habari kwa klabu hiyo, mwenye maneno mengi, Masau Bwire ameiambia MPENJA BLOG kuwa klabu hiyo imefanikiwa
kuwanasa wanandinga watano wenye uzoefu wa hali ya juu katika michuano ya ligi
kuu soka Tanzania bara kwa lengo la kumaliza katika nafasi nzuri msimu ujao.
Masau
alisema klabu hiyo inafuata taratibu zote za uongozi na haifanyi mambo kiholelaholela
kama zinavyofanya klabu zingine zinazoshiriki ligi kuu hususani Simba na Yanga.
“Sisi huwa
tunafanya kazi kutokana na maelekezo ya mwalimu. Kila mmoja aheshimu kazi ya
mwenzake na hapo tutaweza kusonga”. Alisema Masau.
“Mpaka sasa tumeshasajili wachezaji watano
wenye uzoefu na ligi kuu ambao kocha Tom Alex Olaba aliwapendekeza. Wachezaji
hao ni pamoja na Zuberi Dabi kutoka kagera sugar,Salvatory Ntebe,Juma Mpakala
na Yusuf Nguya wote kutoka mtibwa sugar ambao mikataba yao imemalizika, bila kumsahau Muzinga ambaye alikuwa anakipiga
katika ligi ya nchini Burundi” aliongeza Masau Bwire.
Maafande wa
Ruvu shooting walifanikiwa kumaliza nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania
bara msimu uliopita nyuma ya vinara wa ligi, Azam fc, Yanga, Mbeya city, Simba
sc pamoja na wanankulukumbi kagera sugar.
0 comments:
Post a Comment