
Anaondoka? Liverpool na Barcelona wanatarajia kuanza mazungumzo juu ya kuuziana Luis Suarez.
Imechapishwa Julai 2, 2014, saa 6:43 mchana
KLABU
za Liverpool na Barcelona zinatarajia kuanza kufanya mazungumzo juu ya
bei ya awali ya paundi milioni 80 ili kuuziana mshambuliaji mweye
matatizo kwa sasa, Muurguay, Luis Suarez.
Mtandao wa michezo wa Sportsmail unafahamu
kuwa maofisa wa Liverpool, akiwemo mkurugenzi mtendaji, Ian Ayre,
wamekubali kukutana na mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona, Raul
Sanllehi, mjini London ili kujadiliana thamani ya mchezaji huyo mwenye
miaka 27.
Barcelona
wanatazamiwa kutoa paundi milioni 60 kwa kuzingatia kuwa Suarez
amefungiwa miezi minne kucheza soka baada ya kumng`ata beki wa Italia,
Giorgio Chiellini.
Liverpool
hawapo tayari kushusha bei ya Suarez, lakini wanataka kumhusisha
mshambuliaji wa Barcelona Alexis Sanchez kama sehemu ya makubaliano
hayo.

Suarez anahusishwa kujiunga na Barcelona baada ya kufungiwa miezi minne kucheza soka.
Barcelona wanasema mchezaji wao wa kimataifa wa Chile ana thamani ya paundi milioni 35, lakini tayari wameshakataa ofa ya paundi milioni 20 kutoka kwa Juventus ya Italia iliyokuwa na nia ya kumsajili nyota huyo mwenye miaka 25.
0 comments:
Post a Comment