
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 12, 2014, saa 9:40 alasiri
WAKATA miwa wa Kaitaba, Kagera Sugar, rasmi wameanza kambi kujiwinda na mikikimikiki ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange
amezugumza na MPENJA BLOG na
kufafanua kuwa jana walifika Bukoba kambini na leo hii ndio wameanza kusaka kasi
mpya kuelekea msimu mpya.
“Mungu ametusaidia tumefika Bukoba kambini jana,
kwahiyo leo tumeanza kambi yetu rasmi kujiwinda na ligi kuu”. Alisema Kabange.
Kabange aliongeza kuwa kusogezwa mbele kwa
michuano ya ligi kuu ni faraja kwao kwani watapata muda mzuri wa kukijenga
kikosi chao kilichosheheni vijana wapya.
“Ni kweli ligi imesogezwa mpaka septemba 20, kwa
upande mwingine ni nafuu kwetu ili tuweze kujipangga vizuri”.
“kama unavyojua, tuna vijana wengi wapya, kwahiyo
naona kwetu inakuwa faraja, tutaweza
kuwaweka pamoja wachezaji wapya na wa zamani. Tunashukuru kwa kuweza kupata
muda huu ulioongezwa”. Aliongeza Kabange.
Kuhusu matatizo ya kikosi chao msimu uliopita
ambao walishika nafasi ya tano kwa kujikusanyia pointi 38, Kabange alisema: “Sisi
tulikuwa na usumbufu zaidi katika safu ya ushambuliaji, kama ulivyo wimbo wa
Taifa Tanzania, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kuchukua vijana chipukizi
ambao wanaweza kutusaidia kama tulivyowatengeneza”.
“Them Felix `Mnyama` ameondoka kuelekea Mbeya City
fc, tulikuwa na mpango na kocha wangu
kuchukua mshambuliaji kutoka Uganda, lakini mipango hiyo imeshindikana. Kwahiyo
wachezaji tuliowasajili ni Watanzania watupu na naamini tukifanya nao mazoezi
tunaweza kufika pale tulipokusudia”. Alifafanua Kabange.
0 comments:
Post a Comment