
Jerryson Tegere baada ya kuongezewa mkataba na timu yake ya Yanga amewasili mazoezini leo. (Picha na ukurasa wa Facebook wa Yanga sc).



Picha zote zimechukuliwa kutoka ukurasa wa Yanga kwenye mtandao wa Facebook .
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MAKAMU bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara,
klabu ya Yanga ya Dar es salaam imeanza mazoezi ya kujiwinda na msimu wa
2014/2015 wa ligi kuu na kombe la Kagame katika Fukwe za Coco Beach jijini Dar
es salaam.
Mazoezi hayo yapo chini ya kocha wa makipa, Juma
Pondamali `Mensah` wakati huu klabu ikimsubiri kocha mpya, Mbrazil, Marcio
Maximo ambaye anatarajia kuwasili kesho kama mambo yatakwenda kama yalivyangwa.
Mazungumzo ya Maximo na Yanga sc yalisimamiwa na
bosi mwenyewe, Yufus Manji, hivyo kwa asilimia nyingi, Mbrazil huyo mwenye
heshima zaidi nchini Tanzania kutokana
na mafanikio aliyoyapata wakati akiifundisha Taifa stars atatu kukinoa
kikosi hicho chenye masikani yake mtaa wa Jangwani kariokoo jijini Dar es
salaam.
Wakati Yanga wakiendelea kumsubiri Maximo, tayari
aliyekuwa kocha msaidizi, Charles Boniface Mkwasa ameshaondoka na kuelekea
Uarabuni.
Mkwasa amepata kazi nchini Saudi Arabia na taarifa
zilibainisha kuwa ameenda kuungana na aliyekuwa bosi wake Yanga, kocha
mholanzi, Hans Van der Pluijm alitetimka kwa makubaliano baada ya mkataba wake
kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.
Yanga imeweza kuweka wazi majina ya awali ya
baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu.
Msimu
uliopita Yanga ilikuwa na kikosi cha wachezaji 30 kutoka timu ya Wakubwa na
wachezaji watano (5) kutoka timu ya vijana (U20) waliokuwa wamepandishwa
kwa ajili kupata uzoefu na kuiongozea nguvu timu ya wakubwa katika michezo
mbalimbali.
Hata
hivyo kutokana na ripoti ya benchi la ufundi iliyowasilishwa mara baada ya ligi
kumalizika, wachezaji 11 wameachwa katika usajili na tayari uongozi
umemalizikana nao na kuwa huru kutafuta timu nyingine.
Wachezaji
hao ni: David Luhende, Athuman Idd "Chuji", Geroge Banda -U20, Yusuph Abdul -U20, Rehani Kibingu -U20, Hamisi Thabiti, Reliants Lusajo, Bakari Masoud - U20, Shaban Kondo, Abdalllah Mguhi "Messi" U-20 na Ibrahim
Job .
Yanga imewaongezea mikataba ya miaka miwili miwili wachezaji
wake Jerryson John Tegete, Said Bahanuzi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ally
Mustapha `Barthez`, Mbuyu Twite, Juma
Abdul, Oscar Joshua, Simon Msuva.
0 comments:
Post a Comment