
Kocha
Mkuu mpya wa Yanga Marcio Maximo (kushoto)akiwa na Afisa Habari Baraka
Kizuguto, Katibu Mkuu Beno Njovu na kocha msaidizi Leonadro Neiva mara baada ya
kuwasili Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere
Kocha
Mbrazil Marcio Marcel Maximo tayari ameshawasili jijini Dar es salaam kwa ajili
ya kuanza kazi kukinoa kikosi cha timu ya Young Africans kwa ajili ya msimu
ujao kwenye mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya
Kimataifa.
Kocha
Maximo ambaye awali aliwahi kufanya kazi nchini akiwa kama Kocha Mkuu wa timu
ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) amewasili mchana wa leo akiwa na msaidizi wake
Leonadro Martins Neiva kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini na kulakiwa na
umati mkubwa uliokuwa umejitokeza kumlaki.
Mara
baada ya kuwasili kocha Maximo pamoja na msaidizi wake Neiva walipokelewa na
Katibu Mkuu wa Yanga SC Bw. Beno Njovu ambapo mara baada ya kukamilisha masuala
yote ya uhamiaji walitoka nje na kuwapungia mikono washabiki, wapenzi na
wanachama waliokuwepo uwanjani hapo
Kuhus
ujio wake Tanzania kujiunga na klabu ya Yanga SC Maximo alisema kesho ataongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani majira ya
saa 5 kamili asubuhi ambapo ndipo atapata fursa ya kueleza kila kitu juu ya
ujio wake.
Aidha
kesho majra ya saa 8 kamili mchana kiungo mshambuliaji Andrey Macrcel Ferreira
Coutinho anatarajiwa kuwasili kwa shirika la Ndege la Afrka Kusini tayari kwa
ajili ya kujiunga na kikosi cha Young Africans kwenye maandalizi ya msimu mpya
wa 2014/2015.
Wapenzi,
wanachama, na washabiki wa Young Africans mnaombwa kujitokeza kwa wingi Uwanja
wa Ndege wa JK Nyerer kumpokea kiungo huyo ambaye amesema anakuja kufanya kazi
nzuri nchini na kuisaidia Yanga kwenye michuano mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment