
 Oribe Peralta (kushoto) aliwafungia Mexico bao pekee la ushindi katika dakika ya 61.
BAO pekee 
la Oribe Peralta katika dakika ya 61 limetosha kuwapa Mexico ushindi wa 
mechi ya kwanza ya fainali ya kombe la dunia nchini Brazil, lakini bado 
waamuzi wameonekana kuzua hofu kiuwezo
Mwamuzi 
 kutoka Colombia, Wilmar Roldan aliwanyima mabao mawili Mexico katika 
dimba la  Natal Estadio das Dunas kipindi cha kwanza
baada ya kutoa maamuzi ya kuotea kwa mfungaji wa mabao hayo, mchezaji wa
 zamani wa Tottenham Giovani dos Santos.
Lakini
 mambo yalikuwa nafuu kwa Mexico waliotawala mchezo huo baada ya mlinda 
mlango wa Cameroon Charles Itandje kuutema mpira uliopigwa na Dos Santos
 na ukamkuta Peralta akiwa katika nafasi nzuri ambapo hakufanya makosa 
na kuukwamisha mpira nyavuni.
Matokeo
 hayo yanawapa nafasi nzuri  Mexico kufuzu hatua ya 16 bora kutoka kundi
 A sambamba na wenyeji Brazil na timu hizo zitaumana jumanne ya wiki 
ijayo mjini 
 Fortaleza.
Peralta akishangilia bao lake

Wachezaji wa Mexco wakishangilia bao lao usiku huu.

Siku mbaya: Giovani Dos Santos alishuhudia mabao yake mawili yakikataliwa
Kikosi cha Mexico leo: Ochoa, Layun, Moreno, Marquez, Rodriguez, Aguilar, Guardado (Fabian 69'), Vazquez, Herrera, Giovani, Peralta (Hernandez 74'). 
Wachezaji wa akiba: Corona, Salcido, Reyes, Jimenez, Pulido, Ponce, Brizuela, Aquino, Pena, Talavera.
Kdi ya njano: Moreno
Goli: Peralta 61'
Kikosi cha Cameroon: Itandje, Djeugoue (Nounkeu 45'), N'Koulou, Chedjou, Assou-Ekotto, Song (Webo 79'), Mbia, Enoh, Moukandjo, Eto'o, Choupo-Moting.
Wachezaji wa akiba: Feudjou, Aboubakar, Makoun, Bedimo, Fabrice,
Salli, Matip, Nyom, N'Djock.
Kdi: Nounkeu
Mwamuzi: Wilmar Roldan Perez
Idadi ya mashabiki: 39, 216
Kdi ya njano: Moreno
Goli: Peralta 61'
Kikosi cha Cameroon: Itandje, Djeugoue (Nounkeu 45'), N'Koulou, Chedjou, Assou-Ekotto, Song (Webo 79'), Mbia, Enoh, Moukandjo, Eto'o, Choupo-Moting.
Wachezaji wa akiba: Feudjou, Aboubakar, Makoun, Bedimo, Fabrice,
Salli, Matip, Nyom, N'Djock.
Kdi: Nounkeu
Mwamuzi: Wilmar Roldan Perez
Idadi ya mashabiki: 39, 216

Samuel Eto'o alikosa nafasi ya kuifungia bao Cameroon kipindi cha kanza.

Dos Santos (kulia) akifunga bao la pili lakini nalo lilikataliwa na mwamuzi 


0 comments:
Post a Comment