Mchezaji
wa mchezo wa Vishale ‘Darts’ wa Timu ya Mbeya City, Mary Banabas
(kushoto), akirusha mshale katika mashindano ya mchezo huo Ukanda wa
Afrika Mashariki dhidi ya mchezaji Salome Gacheri wa Kenya,
yaliyofanyika Viwanja vya Rose Garden mjini Dodoma jana. Mbeya City
ilishinda kwa mabao 3-2.
Mchezaji Levocatus Siriwa kutoka Magereza Jijini Arusha akirusha mshale katika mashindano hayo.
Mchezaji kutoka Dodoma, Shukurani Dai akirusha mshale katika michuano hiyo.
Mchezaji wa mchezo huo kutoka timu ya Lugalo Tanzania Mr Shawa akirusha mchale katika fainali hizo.
Mzee Carlos Kidilu kutoka Dodoma akishiriki mchezo huo.
Mchezaji Mr Herry kutoka Lugalo Dar es Salaam akirusha mshale.
Mchezaji wa mchezo huo kutoka Dar es Salaam, Julius Mwiru akirusha mshale wakati wa mashindano hayo.
Wachezaji wa mchezo huo wakisubiri kushiriki michuano hiyo.
Dotto Mwaibale, Dodoma
SERIKALI imesema inampango wa kuanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya kuendeleza michezo nchini.
Hayo
yalibainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana Michezo na Utamaduni,
Juma Nkamia wakati akifungua mashindano ya mchezo wa Vishale ya Ukanda
wa Afrika Mashariki’Darts’ mjini Dodoma leo.
“Serikali inatarajia kuanzisha mfuko utakakuwa ikisaidia michezo yote hapa nchini ukiwemo huu wa Vishale” alisema Nkamia.
Alisema
mchezo wa mpira wa miguu ndio umekwa ukipewa kipaumbele zaidi lakini
kupitia mfuko huo utasaidia michezo mingine ikiwemo wa Vishale ambao
umekuwa maarufu hapoa nchini.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania,David Msabi alisema
wamekuwa na changamoto kubwa ya kukosa ufadhili kutoka serikalini na
kuwa mchezo huo unaonekana unachezwa na walevi wakati si kweli.
Alitaja changamoto nyingine ni kukosekana kwa viwanja na walimu wa kufundisha mchezo huo ambao tayari utajitangaza kimataifa.
Katika mashindano hayo timu kutoka nchi za Uganda, Kenya zimeshiriki Tanzania ikiwa ni mwenyeji.
0 comments:
Post a Comment