
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa Simba sc,
Wakili, Dkt. Damas Ndumbaro Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Juni 27, 2014, saa 3:49 alasiri
WEKUNDU
wa Msimbazi Simba wanatarajia kumpata rais mpya, makamu wa rais na wajumbe
wapya wa kamati ya utendaji katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo unaotarajia
kufanyika juni 29 mwaka huu.
Awali
uchaguzi huo uligubikwa na mizengwe hususani baada ya kuenguliwa kwa jina la
mgombea wa Urais, Michael Richard Wambura.
Wambura
alikata rufani mara ya kwanza katika kamati ya rufani ya uchaguzi wa TFF baada
ya kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya mwenyekiti wake, Wakili, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuliengua jina lake
kwenye mchakato wa uchaguzi.
Sababu
kubwa zilizosababisha Wambura kuenguliwa ni kuipeleka Simba mahakamani na
kusimamishwa uanachama mwaka 2010.
Baada
ya kamati ya rufani chini ya Jaji Julius Mutabazi Lugaziya kubaini Simba
walifanya makosa kwa kumuacha Wambura akishiriki shughuli za Simba ikiwemo
kulipia ada wakati walitangaza kumsimamisha, iliamua kumrejesha.
Kamati
ya uchaguzi ya Simba ikaliengua jina la Wambura kwa mara ya pili baada ya
kubainika kuongea maneno ya kampeni kabla ya muda, lakini `kidume` alikata rufani
tena na akachinjwa rasmi na kamati ya rufani ya uchaguzi baada ya kubaini
alifanya makosa.

Wanachama wa Simba huu ndio muda wa kuijenga klabu yenu kwa kupata viongozi bora
Baada
ya mizengwe ya muda mrefu sasa mambo yameiva ambapo leo hii kamati ya Uchaguzi
ya Simba SC imesema kuwa inapenda kuwaalika wanachama wote wa Simba katika
Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu uliopangwa kufanyika Keshokutwa Jumapili,
Juni 29 mwaka huu, katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay
jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na katibu mkuu wa Simba sc,
Ezekiel Kamwaga, shughuli za uhakiki wa wanachama zitaanza saa moja kamili
asubuhi na Mkutano umepangwa kuanza saa tatu kamili asubuhi na wanachama na
wagombea wote wanaombwa kuwa wamekaa katika viti vyao kufikia muda huo.
Kamwaga
alifafanua kuwa katika uchaguzi huo, jumla ya wagombea 27 wanatarajiwa
kushiriki na Kamati ya Uchaguzi imeazimia kwamba suala la muda litazingatiwa
sana safari hii kutokana na ukweli wa kuwepo kwa wagombea wengi.
“Ni matumaini ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kwamba wanachama watazingatia muda wa kufika ili kurahisisha shughuli za kamati”.Ilisema Taarifa ya Kamwaga.
“Ni matumaini ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kwamba wanachama watazingatia muda wa kufika ili kurahisisha shughuli za kamati”.Ilisema Taarifa ya Kamwaga.
“Kamati
inatangaza pia kwamba katika uchaguzi huo, ulinzi utakuwa wa kiwango cha juu;
ingawa ina matumaini kwamba wanachama wote watakuwa watulivu ili kulinda jina,
heshima na hadhi ya Simba SC.
Benki ya Posta”
Benki ya Posta”
Kamwaga
aliongeza kuwa kwamba kwenye uchaguzi kutakuwa pia na huduma ya kutoa kadi kwa
washabiki wa Simba wanaotaka kuingia katika mfumo mpya wa Benki ya Posta.
Simba
na Benki ya Posta zimeingia katika makubaliano ya kutengeneza kadi hizo ambazo
kwa utaratibu utakaotangazwa katika siku zijazo, ndiyo zitatumika kwa wanachama
wote.
0 comments:
Post a Comment