Na
Mwandishi wetu, Tanga
WAZIRI
wa Viwanda na Biashara Dr.Abdallah Kigoda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
mechi ya kirafiki kati ya timu ya vijana ya Coastal Union na Handeni City
utakaochezwa Jumamosi wiki hii wilayani humo.
Mchezo
huo ni moja kati ya mechi mbalimbali za majaribio wanazocheza timu hiyo lengo
likiwa ni kukipa makali kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana ikiwemo
Rolling Stone na mengine yatakayojitokeza.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union,
Salim Bawazir alisema mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa soka Kigoda ambao
awali ulikuwa ukiitwa Azimio kuanzia majira ya saa kumi jioni.
Bawaziri
timu hiyo itaondoka wilaya ya Tanga Jumamosi asubuhi ili kuweza kufika mapema
wilayani humo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mechi hiyo ikiwemo kuwataka
wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi.
“Mchezo huu ni muhimu sana kwa timu yetu ya
vijana kwani wanajiandaa na mashandano mbalimbali hasa yale ya vijana ikiwemo
Rolling Stone na Kombe la Uhai Cup “Alisema Bawaziri .
Katika
hatua nyengine wachezaji wa waliosajiliwa kwenye timu ya Coastal Union ambayo
inashiriki mashindano ya ligi kuu Tanzania bara wanatarajiwa kuwasili mkoani
Tanga muda wowote kuanzia jana.
0 comments:
Post a Comment