Miss Sinza 2013 Prisca Clement katikati mara baada ya kushinda taji la vipaji katika mashindano ya Miss Tanzania 2013
Na Mwandishi Wetu
Waandaaji wa mashindano ya
kumsaka mrembo wa Sinza, Miss 2014 wametoa wito kwa wasichana wenye
vigezo vya kuwania taji la mwaka huu kujitokeza katika mazoezi
yanayoendelea kwenye ukumbi wa Meeda Club uliopo katika barabara ya
Sinza Mori na Lufungila jijini.
Akizungumza jijini jana,
Muandaaji wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa lengo lao ni
kuwa na warembo wengi ili kuwapa nafasi majaji kuchagua washindi ambao
wataiwakilisha vyema Sinza na vitongoji vyake katika mashindano ya Kanda
ya Kinondoni na Miss Tanzania.
Majuto alisema kuwa mpaka sasa
jumla ya warembo nane wamejitokeza katika mazoezi ya mwaka huu, idadi
ambao haitoshi kutokana na malengo yao ambayo ni warembo 20.
Alisema kuwa uwepo wa washindani
wengi, kunatoa changamoto hata kwa majaji na kutoa mrembo bora zaidi na
kuwa mwakilishi wa kweli. “Hatujafunga milango ya kuwapokea warembo,
tunawaomba wafike mazoezini kuanzia saa 10.30 jioni na kukutana na
wakufunzi wetu, Fomu zinatolewa bure,” alisema Majuto.
Majuto pia aliwaomba wadau wa
mashindano ya urembo nchini kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwa
lengo la kuleta maendeleo, kuongeza ushindano mbali ya kutangaza
biashara zao.
Alisema kuwa ni fursa pekee
kudhamini mashindano hayo kutokana na mvuto uliopo, kwani watazamaji
wengi ufika kuangalia mazoezi na wakati wa mashindano.
Taji la Miss Sinza linashikiliwa
na Miss Tanzania, Prisca Clement alimaliza katika hatua ya 10 bora
katika mashindano ya mwaka jana ya Miss Tanzania na pia alishinda taji
la mrembo mwenye kipaji katika mashindano hayo.


0 comments:
Post a Comment