
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kikosi cha timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) chenye watu
25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano
dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).
Mechi hiyo
itachezwa Jumamosi (Mei 24 mwaka huu) katika Jiji la Kaduna kwenye Jimbo la
Kaduna ambalo lipo katikati ya Nigeria. Msafara wa timu hiyo unaoongozwa na
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Ayoub Nyenzi unaondoka kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Ngorongoro
Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza iliyofanyika
nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.
Mwamuzi
Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Atasaidiwa na
Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni
Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.

0 comments:
Post a Comment