
Na Baraka Mpenja
Imechapishwa Mei 25, 22014, saa 4:55 usiku
TP MAZEMBE wamefanikiwa kushinda mchezo wao wa kwanza wa liigi ya mabingwa barani Afrika hatua ya makundi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 leo hii dhidi ya wapinzani wao wakubwa, AS Vita.
Mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki
wengi nchini DR Congo umepigwa mjini Lubumbashi.
Bao pekee la ushindi kwa TP Mazembe
limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta katika
dakika ya 62.
Hata hivyo, Samatta aliyeanza katika
mechi leo alitolewa mnamo dakika ya 82 na nafasi yake kuchukuliwa na Jonas
Sakuwaha.
Katika mchezo wa leo Thomas Ulimwengu
alianzia benchi na kuingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa
kimataifa wa Zambia, Rainford Kalaba.
Mabadiliko hayakuweza kuleta mabadiliko
makubwa katika ubao wa matangazo.
0 comments:
Post a Comment