




Na Mwandishi Wetu
Imechapishwa Mei 25, 2014 saa 1: 54 mchana
Mashindano ya Castle Lager Perfect Six ngazi ya mikoa yameanza
kutimua vumbi wikendi hii ambapo jumla ya timu 48 zimeshuka dimbani
katika mikoa ya Dar na Morogoro zikiwania nafasi ya kufuzu kushiriki
ngazi ya kanda na hatimaye fainali za kitaifa.
Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo alisema kuwa mechi
zilizochezwa wikendi hii zimeonyesha jinsi gani Watanzania wana mwamko
na shauku kubwa ya kushiriki mashindano kutokana na watu kujitokeza kwa
wingi maeneo mbalimbali ambapo yalifanyika mashindano hayo ya kwanza.
Mechi zilizochezwa wikendi hii ilikuwa ni awamu ya kwanza ya
mashindano hayo ambapo timu zitakazofuzu hatua hiyo ya mikoa zitachuana
katika ngazi ya kanda na hatimaye taifa. Washindi wa fainali za taifa
watajipatia fursa ya kipekee kwenda kutembelea jiji la Barcelona huko
Hispania na kuiona timu ya Barcelona ikicheza na pia wataweza kujionea
mambo mbalimbali ya kihistoria katika uwanja wa Camp Nou.
Baadhi ya maeneo na timu zilizoshiriki ni Ilala ambapo timu
zilizoshiriki ni Nato FC, Gaddafi FC, Barafu Veterani, Pata Habari, Dira
ya Mtanzania, Hazard Team, Mburahati Veterans na Baracuda FC ambapo
mechi hizo zilipigwa kwenye uwanja wa Rova Ashanti na Baracudda FC
waliibuka washindi. Temeke ni Lumo FC, Sunset FC, Flamingo FC, Yombo
Classic, Wazee wa Povu FC, Shelly FC, Mwisho wa Lami FC, na Oilcom FC
ambapo mechi hizo zilipigwa kwenye uwanja wa Mwembeyanga na Gaddafi
kuibuka washindi. Kwa mechi iliyochezwa uwanja wa Mwinjuma Kinondoni
timu ya AUCT iliibuka washindi. Fainali za kanda ya Dar es salaam
zitachezwa Juni 8 kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe ambapo timu
zilizofuzu Temeke, Ilala na Kinondoni zitachuana kupata washindi
watakaoshiriki fainali za taifa.
Na huko Morogoro, timu za soka za Mzinga FC na Ndezi FC
zimefanikiwa kutinga hatua ya fainali za kanda ya mashariki baada ya
kufanya vizuri mashindano hayo yaliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi
Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika
kwa michezo iliyoshirikisha timu nane mjini hapa, Mwamuzi wa mchezo huo
Elly Sasii alisema kuwa ni timu za Mzinga na Ndezi ndizo zilizofanikiwa
kutinga hatua ya fainali za kanda ya mashariki ikisubiri washindi
wenzao wa mkoa wa Dodoma.
Sasii alisema kuwa Mzinga na Ndezi zitacheza ligi ndogo ya
mashindano hayo Juni 7 mwaka huu Manispaa ya Morogoro na washindi wa
Dodoma ili kupata timu moja itayowakilisha kanda ya mashariki katika
mashindano ya taifa yatayofanyika baadaye jijini Dar es Saalaam.
“Haya mashindano hapa nchini ni mapya na lengo lake ni kupata
timu moja itayoenda Hispania kushuhudia michezo ya Barcelona.”alisema
Sasii.
Sasii alifafanua kuwa washindi hayo walifanikiwa kushinda timu
nyingine katika hatua ya mtoano, robo fainali ikihusisha timu za
Misufini A na B, Nyumbani Park A na B, Airport Rangers na Mtazamo zote
za Manispaa ya Morogoro.
Kanda zitakachuana ni pamoja na kanda ya mashariki, Kaskazi,
kanda ya Ziwa na kanda za nyanda za juu kusini ambapo baadhi ya kanda
michuano hiyo tayari zimeanza rasmi mei 24 mwaka.
0 comments:
Post a Comment