Thursday, April 17, 2014

LIVERPOOL hawajabeba taji kwa miaka 24 sasa na msimu huu wapo katika kinyang`anyiro cha ubingwa wa ligi kuu soka nchini England, huku vita yake ikiwa ni dhidi ya Chelsea na Manchester City.
Majogoo wa jiji mpaka sasa wana pointi 77 kileleni, baada ya kucheza mechi 34. Nafasi ya pili wapo Chelsea wenye pointi 75 baada ya kushuka dimbani mara 34, huku Manchester City wakishika nafasi ya tatu kwa poointi 71 kwa mechi 33 walizocheza.
Luis Suarez na Daniel Strurridge wamekuwa washambuliaji muhimu mno kwa Liverpool katika safari yao ya kuisaka ndoo baada ya miaka mingi kupita.
Lakini taarifa mbaya kwa mashabiki wa wekundu hawa wa Anfield kuelekea mchezo wa ugenini jumapili dhidi ya Norwich ni kwamba Sturridge yuko hatarini kuukosa kutokana na maumivu ya misuli aliyonayo.
Mshambuliaji huyo raia wa Uingereza alitolewa katika dakika ya 66 kwenye mchezo walioshinda mabao 3-1 dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki iliyopita na baadaye kugundulika ana maamuzi ya nyama za paja.
Taarifa rasmi kutoka katika mtandao wa Liverpool inasema;
“Sturridge anaendelea na matibabu na yupo katika uangalizi mkubwa chini ya madaktari wa timu Melwood na aligundulika kuwa na maamivu kidogo”.
Nyota huyo mwenye miaka 24 na aliyewahi kuzichezea Chelsea na Manchester City amefunga mabao 20 msimu huu na kutengeneza ushirikiano mzuri na nyota raia wa Uruguay, Luis Suarez na kukaribia kutwaa ubingwa.
Baada ya mechi ya ugenini dhidi ya Norwich, Liverpool watawakaribisha Chelsea, baadaye Crystal Palace na watamaliza kampeni zake nyumbani dhidi ya Newcastle United.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video