AMEKUWA
katika wakati mgumu kutokana na kupoteza makali yake ya kufunga baada
ya kutua Chelsea kwa dau la rekodi, Pauni Milioni 50 katika usajili wa
Januari 31, mwaka 2011.
Akiwa
amefunga mabao tisa tu msimu huu, bao lake la mwisho katika Ligi Kuu
England akiwa amefunga Januari 11, inamaanisha Fernando Torres - pamoja
na wachezaji wenzake kadhaa walioshuka viwango Chelsea watakuwa mstari
wa mbele kuuzwa kwa mujibu wa mipango ya kocha Jose Mourinho.
Kocha
huyo Mreno alimkandia mshambuliaji huyo baada ya mechi ya kwanza ya
Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakifungwa 3-1 na Paris
Saint-Germain nchini Ufaransa na ameweka wazi atamuuza.
Lakini
Torres amepogwa picha akishiriki kampeni ya kuzitangaza jezi mpya za
Chelsea ijulikanayo kama 'Forever Blue', na je, hiyo maana yake
Mspanyola huyo atabaki Stamford Bridge msimu ujao?

Kampeni:
Fernando Torres ametumika katika kampeni ya uzinduzi wa jezi mpya za
Chelsea, hiyo inamaanisha atabaki katika klabu hiyo?


0 comments:
Post a Comment