
BAADA
 ya suluhu pacha ya bila kufungana ( 0-0) na Chelsea, nahodha wa 
Atletioc Madrid, Gabi amekerwa na mbinu ya `kupaki basi` waliyotumia 
wapinzani wao katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, ligi ya mabingwa 
barani Ulaya.
Atletico
 wanaosifiwa kujilinda katika ligi ya Hispania, La Liga wamekutana na 
Chelsea ambayo ina uwezo mkubwa wa  `Kupaki basi` kwenye ligi ya 
England.
Katika
 nusu fainali hii ambayo haitasahaulika kwa Atletico, vinara hao wa La 
Liga  walimiliki mpira kwa asilima 62 na kupiga mashuti 26 golini, 
wakati Chelsea walipiga mashuti matano tu.
Matokoe
 ya leo yanaonekana kuwa mazuri kuelekea mechi ya marudiano darajani, 
ambapo washambiliaji wawili wa Chelsea Eden Hazard na Samuel Eto`o 
watarejea uwanjani.
Gabi amekiri kuwa matokeo ya leo yamewaacha katika hatari kubwa.
“Hatujaridhika, lakini mechi bado. Atletico walihitaji kushinda kutoka mwanzo wa mchezo hadi mwisho”.
“ Tulijua Chelsea wasingekubali kufungwa kirahisi na mwisho wa siku tumetoka kapa”. Gabi amewaambia waandishi wa habari.
Atletico
 hawajafungwa katika michuano ya kimataifa mwaka huu, lakini matokeo ya 
leo yamewafanya washindwe kupata ushindi kwa mara ya kwanza katika 
michuano ya ulaya msimu huu wa 2013/2014.
Katika
 mechi ya leo, Chelsea wamepatwa na majanga baada ya nahodha wake, John 
Terry  na mlinda mlango namba moja, Petr Cech kupata majeruhi.
 K
 Leo nusu fainali ya pili itashuhudiwa katika dimba la Santiago Bernabeu 
ambapo Real Madrid watawakaribisha mabingwa watetezi, Bayern Munich.
K
 Leo nusu fainali ya pili itashuhudiwa katika dimba la Santiago Bernabeu 
ambapo Real Madrid watawakaribisha mabingwa watetezi, Bayern Munich.
Hii inatazamiwa kuwa nusu fainali ya dunia kutokana na ukubwa wa klabu hizi mbili.




0 comments:
Post a Comment