DROO ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imekalimika muda mfupi uliopita ambapo Manchester United wameangukia mikononi mwa mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich.
Timu pekee nyingine ya England iliyosalia UEFA, Chelsea yenyewe imepangiwa mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain baada ya chungu kuzungushwa na nyota wa zamani wa Ureno Luis Figo.
FC Barcelona imepangwa kuumana na timu iyocheza nayo ligi moja, Atletico Madrid, wakati Real Madrid wataoneshana kazi dhidi ya wakali wengine wa Bundesliga, Borussia Dortmund.

Mwari huyo!: Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya likiwa limewekwa Nyon, Switzerland wakati wa droo mchana huu

DROO YA ROBO FAINALI IMEMALIZIKA HIVI
Barcelona vs Atletico Madrid
Real Madrid vs Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain vs Chelsea
Manchester United vs Bayern Munich
Mechi za kwanza zitachezwa mwezi wa nne tarehe 1 na 2, wakati mechi za marudiano zitapigwa mwezi wa nne tarehe 8 na 9.
David Moyes alifuzu kwa juhudi kubwa baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Olympiacos dimba Old Trafford ambapo mechi ya kwanza nchini Ugiriki alipigwa 2-0. Lakini sasa amepewa kazi nyingine ngumu zaidi kama anataka kufuzu nusu fainali.
Moyes ambaye bado yupo katika msongo wa mawaza kufuatia kipiga cha 3-0 kutoka kwa Liverpool wiki iliyopita, atakutana na kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola ambaye sasa yupo Allianz Arena.
Bayern ambao waliwatupa nje Man United mwaka 2010 walikuwa wa kwanza katika kundi lao lililokuwa na klabu za Manchester City, CSKA Moscow na Viktoria Plzen.

Amefurahi? Samuel Eto’o na Chelsea yake wameliwatoa Galatasaray baada ya kuwafumua mabao 2-0 uwanjani Stamford Bridge hatua ya 16.

Vijana wakubwa: Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (kulia) na Gareth Bale wanatafuta kombe lingine

Mabingwa watetezi!: Bayern Munich walifuzu robo fainali baada ya kuwalowesha Arsenal


Usitusamehe: Lionel Messi na Barcelona yake waliwatungua Manchester City na kufuzu robo fainali
PICHA NA SPORTSMAIL
0 comments:
Post a Comment