Sunday, March 23, 2014

Na Omary sadick Kuhanzibwa.

Wakati uso wasaa ya dunia unaenda kasi sana, huku nao wana sayansi wakiumiza kichwa kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea, nayo Brazili ikiwa na maombolezo ya nahodha wake  aliyewaisaidia kutwaa kombe la dunia pale Sweeden  1950 , wakati huo huo sherehe ya mzee Arsene wenger kutimiza mechi 1000 zikishereheshwa kwa kipgo kibaya cha goli 6-0 kutoka kwa Chalsea, bado uso wa saa wa dunia ukasema kwa nini Manchester United wakiwa mabingwa wa EPL wasistahili kukutana na bingwa mwingine wa Bundesliga ,Bayern Munchen.  The Bavarians.



 Luis Figo,  nguli wa zamanI wa Barcelona , Real Madrid na Ureno huenda ameingia kwenye orodha ya watu ambao pengine wanachukiwa na mashabiki wa Man u, hiii ni kutokana na Droo ya robo fainali ambayo Figo alikuwa balozi wake .



Katika droo hiyo,  klabu ya Manchester United imepangwa kucheza na bingwa mtetezi  wa kombe hilo Buyern Munich, huku wenzao Chelsea wakipangwa dhidi ya Paris saint Germain ya nchini ufarasa.



Lakini tukio lililoshika hisia za watu wengi, na kuchafua mapumziko ya mwisho ya wiki kwa mashabiki ni hili la  Mancheste united.



 Mashabiki  wengi kama sio wote, wakurugenzi, hata jopo la ufundi la Man United, na hata wachambuzi na waandishi mbali mbali wa habari za michezo wasingetamani  Mashetani wekundu  kwa hali waliyo nayo  kukutana na  Bayern ya Pep Guardiola.

Kweli Man United ataweza kuwatafuna wanaume hawa?

Si  kwamba timu hizi ndio zinakutana kwa mara ya kwanza, la hasha..! kwa mujibu wa vyanzo vya habari,   timu hizi zimekutana takribani mara 9.



 Manchester United imefanikiwa kushinda mara 2, kutoka sare mara  4 na kufungwa mara 3,  huku tukio linalokumbukwa na watu wengi na linalowapa matumaini si mashabiki hata wachezaji wa sasa wa Man United na viongozi wao, ni hili la mwaka 1999 katika fainali hizo ambapo Manchester ikiwa chini ya koch Sir Alex Ferguson ilishinda na kutwaa taji hilo.
Holy grail: The Champions League trophy in Nyon, Switzerland ahead of the draw
Mwari huyo!: Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya likiwa limewekwa  Nyon, Switzerland wakati wa droo 


Mara ya mwisho kukutana ni mwaka 2010 katika hutua kama hii ambapo Manchester United waliondoshwa kwa goli la ugenini,  lakini kutokana na hali ya sasa ya Manchester united ambayo ni mbaya, wapo nafasi ya saba kulinganisha na hawa ambao wameshafikia asiliia 99 kutwaa ubingwa nchini kwao na hivyo kuhamishia mawazo yote katika kutetea ubingwa huo wa ligi ya mabingwa barani ulaya, kumesababisha mchezo huo kuwa gumzo katika medani ya soka.


Pamoja na hayo yote mpira ni dakika 90, mpira ni mchezo wa maajabu makubwa. Kuna wakati timu ambayo haipewi nafasi inaweza kufanya maajabu.



Kuna baadhi ya matukio ya kihistoria katika medani hii ya soka yaliyopata kutokea mfano wake ni haya yafuatayo;



Tukianza hapa barani Afrika maeneo ya afrika mashariki nchini Tanzania tunaikuta klabu moja ya simba ya jijin dare s salaam.



Mnamo mwaka 2003, katika michuano ya klabu bingwa afrika, Simba ilipangwa kucheza dhidi ya bingwa mtetezi, klabu ya Zamaleck ya nchini Misiri.



Kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe watu wengi hata Wamisri nao waliamini watasonga mbele hii ni kwasababu timu ya Simba haikupewa nafasi kubwa kutokana na kikosi bora cha wapinzani wao.



Wakati huo Simba ilikuwa na wakali kama akina Suleiman Matola, Emmanuel Gabrile Mwakyusa, beki mahiri Boniphace Pawasa, Victor Costa Nyumba,  Juma kaseja, na wengene wengi chini ya kocha Mkenya James Agrey Siang’a.

In the mix: Wayne Rooney and Manchester United are outsiders for the competition after scraping throughWamevurugwa: Wayne Rooney na  Manchester United watautafuna mfupa wa Bayern Munich?


Si kwamba Simba walikuwa na kikosi kibovu, kikosi chao kilikuwa imara lakini si kama kile cha wapInzani wao, mwisho wa siku Simba ilisonga mbele na kufanikiwa kuingia hatua ya makundi.



Hata huko barani ulaya, nani aliyeamini kuwa Chelsea wanaweza kutwaa taji hilo? mashabiki wengi wa Chelsea walikata tamaa toka hatua ya nusu fainali waliposikia wamepangiwa Barcelona,  lakini mwisho wa siku walitinga fainali wakacheza dhidi ya kikosi hiki kinachoenda kucheza dhidi ya manichester united hatua ya robo fainali.



Goli zuri la Didier  Drogba liliitoa matumaini ya kutwaa taji hilo kwa kuifunga Bayern kwa njia ya penati kutokana na timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1 kwa 1.



Mpira si uchawi wala si maneno, bali ni mbinu unazozitumia  dhidi ya wapinzani wako, hata uwe na kikosi bora zaidi lakini  kama ukikosa mbinu ya kukitumia kikosi hicho, sitashangaaa kutokea kama yale yaliyotokea kwa simba dhidi ya zamaleck, au Chelsea na Bayern Munich  2012.



 Wachambuzi wengi wa soka wanaikosoa  MAN U .kwamba imeshuka morali na kiongozi wawapo uwanjan , na wamekuwa wakikosoa mbinu na mfumo usioeleweka wa kocha Moyes , kitu ambacho kitampa ugumu mwalimu mwenye falsafa ya `tikitaka` Pep Guardiola  kujua ni mfumo upi unastahili kuwakabili man U..



Maajabu ya Man U kupindua matokea ambayo yamekuwa kama miujiza kwa wengi ambao waliona ni kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano , baada ya mchezo wa kwanza kulala 2 -0 na Olympiakos kule Ugiriki na kufuatiwa na kiwango cha hali ya juu cha wachezaji kama Giggs,Valencia, Rooney , Ferdinand na  Robin Van Persie ambaye kwa bahati mbaya hatakuwepo kwenye michezo yote miwili ya mikondo ya robo fainali.



Inawezekana kwamba Man U  inayopewa nafasi finyu inaweza kuiondoa Bayern ambayo inatazamiwa kuwepo pale Porto katika fainal na kunyakua tena kombe hilo .

2 comments:

Anonymous said...

Sio kweli kwamba Chelsea walikata tamaa baada ya kupangiwa kukutana na Barcelona.Je wajua ni timu katika EPL inayo itesa Barcelona,ni Chelsea wazee wa darajani.Kwahi hiyo Man U wanaouwezo wa kuwapiga Baryen Munich.
Mpira wa miguu ni mchezo wa ajabu yule umzaniae kuwa ndie mara nyingine huwa siyo.Ni mtazamo wangu tu huo,siku njema.

baraka adson said...

Asante kwa maoni yako. Tunashukuru sana na karibu sana

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video