Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976
au 0764302954
KIKOSI
cha wagonga nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City kimeondoka leo asubuhi jijini
Mbeya kuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujiandaa mapema na mchezo wake
dhidi ya Ruvu JKT machi 22 mwaka huu
uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu hiyo, Freddy Jackson wachezaji wote wapo katika hali nzuri tayari
kwa mchezo huo isipokuwa mchezaji Richard Peter ambaye ataukosa mchezo
kwasababau hali yake haijatengamaa baada ya kuumia katika mechi yao dhidi ya Rhino
Rangers ya Tabora uwanja wa sokoine siku za karibuni.
Imeelezwa kuwa Peter bado ana maumivu ya kawaida katika mbavu zake.
“Maandalizi
yetu ni mazuri sana. Tumejiandaa kikamilifu, tupo kamili kuzinyakua pointi tatu. Nayasema
haya kutoka kwa kocha Juma Mwambusi”.
“Kocha
anasema kikosi chake kina uwezo mkubwa sana wa kuibuka na ushindi katika mchezo
huo”. Alisema Jackson katika taarifa yake asubuhi hii.
Kwa niaba ya club, Jackson
aliweka wazi kuwa watakuwa makini
sana na mchezo huu maana wamekuwa wakioneshwa michezo mibaya sana , hasa kwa
hizi timu za majeshi wanapokutana nazo.
“Mfano mzuri ni mchezo wetu dhidi ya Rhino Rangers, wachezaji wetu waliumizwa kwa makusudi kabisa.
Pia tutakuwa makini zaidi na maamuzi ya marefa. Tunaomba mwamuzi atakaechezesha
mchezo huo kuzingatia kanuni na sheria uwanjani ili kutoa haki kwa pande zote
mbili”. Alisema Jackson.
Aidha aliwaomba mashabiki wao kuendelea kuwaamini maana bado wanayo nafasi nzuri ya
kutwaa ubingwa.
Mbeya City wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara wakiwa na
pointi 39, sawa na Yanga waliopo nafasi ya pili kwa pointi 39, lakini tafouti
yao ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Mpaka sasa Mbeya City wameshuka dimbani mara 21, wakati
Yanga wao wamecheza mechi 18.
0 comments:
Post a Comment