Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
WAKIWA na machungu ya kutolewa katika michuano ya
kimataifa, mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Young Africans,
kesho watahamishia hasira zao kwa Mtibwa Sugar katika mechi ya ligi kuu uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro.
Yanga wataingia kwa nguvu zote ili kupunguza maumivu
waliyopata huko Alexndria nchini Misri kufuatia kutupwa nje ya ligi ya mabingwa
barani Afrika na Al Alhy ya Misri kwa penati 4-3.
Mchezo wa
kesho unatazamiwa kuwa mgumu sana kutokana na mazingira ya timu zote mbili.
Mtibwa Sugar wanahitaji ushindi ili kusogea mbele
katika msimamo kwani mpaka sasa wapo nafasi ya 8 wakiwa na pointi 25 ambapo
wameshuka dimbani mara 20.
Msimu huu wana TamTam hao chini ya kocha Mecky
Mexime hajawa na makali ya kutosha, hivyo kesho wataingia uwanjani kutafuta
ushindi mbele ya mabingwa watetezi, ili angalau kujisogeza mbele.
Kwa upande wa Yanga wanahitaji kurejea kileleni mwa
ligi kuu soka Tanzania bara kwani mpaka sasa wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi
38, huku juu yake akiwepo Mbeya City pointi 39 na kileleni wapo Azam fc wenye
pointi 40.
Faida kwa Yanga ni kwamba wamecheza mechi 17 mpaka
sasa, wakati Mbeya City wameshuka dimbani mara 21, na Azam fc amecheza mechi 18
mpaka sasa.
Pia Yanga wana kikosi bora kuliko Mtibwa Sugar, hivyo
wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, lakini imekuwa ngumu sana kwa
wakata miwa kukubali kipigo kutoka kwa timu kubwa za Simba na Yanga.
Mashabiki wa Yanga wanahitaji kuona kiwango cha
klabu hiyo kilichooneshwa kwenye mechi mbili zilizopita dhidi ya Al Ahly.
Yanga ilicheza mpira mkubwa sana katika mchezo wa
machi mosi jijini Dar es saalam na mechi ya marudiano nchini Misri ambapo
walifungwa bao 1-0 ndani ya muda wa kawaida na kutolewa kwa penati 4-3 kufuatia
wastani wa mabao kuwa 1-1 ukizingatia Yanga nao walishinda bao 1-0 uwanja wa
Taifa.
Nao vinara wa ligi kuu, Azam fc watakuwa na kibarua
dhidi ya wagosi wa Kaya katika dimba la Azam complex, Chamazi, nje kidogo ya
jiji la Dar es salaam.
Endapo Azam fc wenye pointi 40 watapoteza mchezo na
Yanga watashinda, basi wanajangwani watarejea kileleni.
Lakini kama Azam fc itashinda na Yanga itashinda,
basi Azam fc wataendelea kubarizi kileleni kama kawaida kwani Yanga atakuwa na
pointi 41 na Azam fc pointi 43.
Kama Yanga
atafungwa kesho, na Azam akafungwa, msimamo utabaki kama ulivyo sasa. Azam
watakuwa kileleni kwa pointi 40, Mbeya City nafasi ya pili pointi 39 na Yanga
nafasi ya tatu pointi 38.
Endapo Yanga atatoka sare kesho na Azam atashinda,
maana yake, Mbeya City ataporomoka kwa nafasi moja kutoka ya pili kwenda ya
tatu kwakuwa Yanga ana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa japokuwa
pointi zitafungana.
Kwa mazingira hayo, mechi za kesho ni ngumu sana kwa
Yanga na Azam fc kutokana na ubora wa Mtibwa Sugar na Coastal Union.
Tayari Yanga wapo Morogoro na wachezaji waliosafiri
ni;
Walinda Mlango:
Deo Munish "Dida", Juma Kaseja na All Mustafa "Barthez"
Walinzi:
Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Nadir Haroub
"Cannavaro", Kelvin Yondani na Ibrahim Job
Viungo: Frank
Domayo, Athumani Idd "Chuji", Nizar Khalfani, Hassan Dilunga na
Haruna Niyonzima
Washambuliaji:
Saimon Msuva, Said Bahanuzi, Hamis Kizza, Emmanuel Okwi, Didier Kavumbagu,
Hussein Javu na Jerson Tegete
0 comments:
Post a Comment