Na Mwandishi Wetu
WAIMBAJI wa miondoko ya muziki wa Injili wa Kufokafoka ‘Gospel Hip Hop’ wametoa wito kwa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya Tamasha kuelekeza nguvu zake katika miondoko hiyo.
Kwa mujibu wa mwimbaji wa nyimbo hizo, Faraja Kampambe ‘Hurukweli’ Msama ni mfano wa kuigwa katika muziki wa Injili ambao unafikisha ujumbe wa Neno la Mungu kwa Jamii.
Hurukweli alisema Msama anatakiwa kugeukia katika miondoko hiyo ili kupata ladha tofauti ya ufikishaji wa huduma ya Neno kwa Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje.
Aidha Hurukweli alisema wakati akimuomba Msama aelekeze nguvu kwenye miondoko hiyo, hivi sasa amekamilisha albam ya nyimbo nane alizorekodi katika studio za K Production ya Tabata na Pantu iliyoko Sinza jijini Dar es Salaam.
Hurukweli anaitaja albam hiyo ni Kila Mwenye pumzi, nyimbo nyingine ni saa ya wokovu, Upendo wa Yesu, Nitarap tu, Sauti hii, My Life, Let it Go na Zinduka.
0 comments:
Post a Comment