
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Tel: o712461976 au 0764302956
YANGA ya Dar es salaam imejitumbukiza kwenye mkataba wa kuuza haki za Matangazo ya Televisheni katika mashindano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kampuni ya Ufaransa ijulikanayo kwa jina la SGM ambao utaanzIa mchezo ya raundi ya kwanza dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.
Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu, amewaambiwa waandishi wa habari mchana wa leo makao makuu ya klabu hiyo, Jangwani, kuwa kampuni ya SGM ina matumaini makubwa kuwa klabu hiyo itapita raundi ya Awali dhidi ya timu dhaifu ya Komorozine ya Comoro na kwenda kuchuana na miamba ya soka barani Afrika, Al Ahly katika Raundi ya Kwanza.
Njovu amesema haki za matangazo ya Television za mechi ya ugenini , Kampuni ya MGB ya Cairo itarusha matangazo hayo kwa nchi za kaskazini mwa Afrika na mashariki ya kati pekee, lakini watawasiliana na wenyeji ili kurusha mechi hiyo kwa Tanzania pekee ili wapenzi wa Yanga wapate burudani.
Njovu amesema mkataba huo utaiwezesha Yanga kupata dola za Kimarekani elfu hamsini na tano (55,000) kwa mechi moja tu ya nyumbani ambazo kwa shilinigi za Kitanzaniani ni zaidi ya Sh. Milioni 90.
Njovu ametoa ruksa kwa kampuni za Kitanzania kupata haki za matanganzo ya mechi hizo, lakini lazima ziwasiliane na SGM kupata ruksa hiyo.
Naye mwakilishi wa SGM, Francis Gaitho amesema kwamba wao wamejiridhisha kuwa Yanga itawatoa nishai Wacomoro na ndio maana wameamua kununua haki hizo mapema.
Yanga ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano mikubwa ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kutwaa ubingwa msimu uliopita wakiwapokonya wapinzani wao wa jadi, klabu ya Simba ya Dar es salaam.
Wanajangwani hao chini ya kocha wake mkuu, Mholanzi, Ernie Brandts wataanza raundi ya awali kwa kukabiliana na Komorozine ya Comoro .
Wakivuka hapo, watatumbukia kwenye kibarua kizito dhidi ya Mabingwa wa Afrika Al Ahly katika Raundi ya Kwanza.
Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Febaruai 7, 8 na 9, na mitanange ya marudiano itakuwa kati ya Februari 14, 15 na 16 February mwakani.
Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Febaruai 7, 8 na 9, na mitanange ya marudiano itakuwa kati ya Februari 14, 15 na 16 February mwakani.
Ili kuhakikisha wanafanya vizuri, Yanga wamefanya usajili wa wachezaji mahiri ikiwemo Mlinda Mlango namba moja Tanzania, Juma Kaseja, Kiungo Kinda, Hassan Dilingu na karibuni walitangaza kumsajili, Emmanuel Anord Okwi kutoka SC Villa Ya Uganda.
Mbali na Okwi, Pia wapo wachezaji wengine wanne ambao ni Beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima, washambuliaji, Didier Kavumbagu na Khamis Friday Kiiza.
Kwasasa Yanga wapo chimbo kujiandaa na mchezo wa Nani Mtani Jembe utakaopigwa keshokutwa uwanja wa Taifa dhidi ya Mabingwa wa zamani wa Tanzania, Simba sc.
0 comments:
Post a Comment