UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA INFORMATION SERVICES
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anapenda kutoa mwaliko kwa makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwasilisha orodha ya watu wasiopungua wanne na waziozidi tisa kwa ajili ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2A) cha kifungu cha 22 cha sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sura ya 83 kinachomtaka Rais kuwaalika kila kundi lililoainishwa chini ya kifungu kidogo cha (1) (c) kutoka pande zote za Muungano kuwasilisha kwake orodha ya majina yasiyopungua 4 na yasiozidi 9 kwa ajili ya kuzingatiwa katika uteuzi.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:
- Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
- Taasisi za kidini
- Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
- Taasisi za elimu ya juu
- Makundi yenye ulemavu
- Vyama vya wafanyakazi
- Vyama vinavyowakilisha wafugaji
- Vyama vya wakulima
- Vyama vinavyowakilisha wavuvi
- Makundi mengine yenye malengo yanayofanana
Katika kuwasilisha majina hayo, makundi yaliyoalikwa yatalazimika kuonesha umri, jinsia, uzoefu, sifa na sehemu ya makazi ya mtu aliyependekezwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia.
Mheshimiwa Rais ameelekeza kuwa orodha ya majina yanayopendekezwa yawasilishwe kwa maandishi ama kwa kupeleka kwa mkono au kutumia huduma ya posta kwa anuani zifuatazo:
- Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais, Ikulu,
S.L.P. 9120,
DAR ES SALAAM
- Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais,
S.L.P. 4224,
ZANZIBAR
Mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo nitarehe 02 Januari, 2014
0 comments:
Post a Comment