Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
MANCHESTER United wanaamini kuwa mshambuliaji wao Wayne Mark Rooney yuko tayari kwa mazungunmzo ya mkataba mpya wa miaka minne utakaogharimu thamani ya pauni milioni 50.
David Moyes anajiandaa kuongeza nguvu katika kikosi chake katika dirisha dogo la usajili (Januari mwakani) ili kuweza kuendana na kasi ya msimu huu ambao Man United inasuasua sana.
Mwenyekiti wa United Ed Woodward amewasiliana mara kadhaa na wakala wa Roney, Bwana Paul Stretford na inafahamika kuwa kikao rasmi kitafanyika siku chache zijazo.

Ni mara ya kwanza kwa klabu kutoa taarifa hiyo tangu kuvunjika kwa mahusiano mazuri baina ya kocha wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson na Rooney ambapo kibabu alisema nyota huyo, 28, aliomba kuondoka, lakini mchezaji huyo mara zote anakataa maneno hayo.
Taarifa za kubakia kwa Rooney zinampa raha Moyes ambaye anataka kuwatoa kafara baadhi ya wachezaji na kusajili wapya ili kuimarisha kikosi chake.
Ashley Young, Nani na Antonio Valencia bado wanajitahidi kutafuta njia ya kubaki na Moyes amesema: ‘Wachache wanaweza kuondoka kama tutapata ofa nzuri.’


Wachezaji wawili wa England Tom Cleverley na Danny Welbeck, pia Javier Hernandez, Anderson na Alex Buttner, hawajathibitisha kubaki au la, wakati Mkongwe Rio Ferdinand na Patrice Evra inaonekana klabu haina mpango wa kuwapa ofa ya mkataba mpya
“Nimejaribu kutoa nafasi kwa kila mtu; alisema Moyes. “Tutauza?, Kama tutapata ofa nzuri pengine tutaangalia hilo”.



”Tutajaribu kuweka usawa kwa kuondoa watu, lakini pia kuwaleta watu”. Alisema Moyes.
Moyes anatupia ndoana zake kwa kiungo wa Atletico Madrid, Koke Face, kwa dau la pauni milioni 15, pia beki wa Porto, Eliaquim Mangala aliowaona kwenye michuano ya UEFA jumatano ya wiki hii. Pia anafanya mipango ya kutuma tena ofa kwa beki wa kushoto wa Everton, Leighton Baines.
0 comments:
Post a Comment