Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MANCHESTER united atavaana na Sunderland katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la ligi wakati Manchester City itapambana na wagonga nyundo wa London, West Ham.
David Moyes alitinga hatua hiyo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stoke City jana usiku, mabao yakifungwa na Ashley Young dakika ya 61 pamoja na beki wa kushoto Patrice Evra dakika ya 78 .
Sunderland waliifunga Chelsea mabao 2-1 siku ya jumanne, huku Ki Sung-Yueng akifunga bao la ushindi dakika za mwisho za muda wa nyongeza.

Katika mchezo mwingine, mshambuliaji Emmanuel Adebayor alirejea uwanjani na kufunga bao moja wakati timu yake, Tottenham Hotspur ikifungwa 2-1 na West Ham United, mabao ya Jarvis dakika ya 80 na Maiga dakika ya 85.
Man United sasa itamenyana na Sunderland katika Nusu Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Capital One, wakati West Ham itakipiga na Manchester City.
Man United sasa itamenyana na Sunderland katika Nusu Fainali ya michuano hiyo maarufu kama Capital One, wakati West Ham itakipiga na Manchester City.


0 comments:
Post a Comment