Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
LIGI kuu soka nchini England (EPL) imeendelea usiku huu kwa mechi moja kubwa kupigwa baina ya washika bunduki wa London, klabu ya Asernal dhidi ya Chelsea.
Kipute hicho kimepigwa katika dimba la Emirates na kushuhudia timu hizo zikitoka suluhu pacha ya bila kufungana (0-0).
Mchezo wa leo ulikuwa muhimu kupata ushindi kwa kocha Aserne Wenger, kwani amekutana zaidi ya mara 10 na Mourinho wote wakiwa makocha na kushindwa kupata matokeo ya ushindi.
Asernal walicheza vizuri na kufika mara kadhaa katika eneo la hatari la Chelsea, lakini walishindwa kutikisha nyavu za wapinzani wao.
Ulikuwa usiku mzuri kwa Mourinho, kikosi chake kilicheza vizuri sana na kuonesha uimara, lakini mipango yake ilikataa.
Pia mechi hii ilikuwa muhimu kwa Asernal kwani walitakiwa kushinda ili kurejea kileleni mwa msimamo wa EPL baada ya Liverpool kushinda wikiendi na kushikilia usukani kwa kujikusanyia pointi 36.
Kwa matokeo ya suluhu, Asernal wanabakia nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 36 sawa na Liverpool, lakini wanazidiwa kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Sasa Majogoo wa jiji wanaojivunia ubora wa Luis Suarez wanaendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu soka nchini England na wengine wakiisoma namba.

Nafasi ya tatu inakaliwa na Manchester City wenye pointi 35, huku Chelsea wakibakia katika nafasi yao ya nne kwa pointi 34, sawa na Everton waliopo katika nafasi ya tano, lakini tofauti ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Mabingwa watetezi, Manchester United wapo nafasi ya nane na pointi zao 28 na juu yake yupo Tottenham Hospurs mwenye pointi 30.
Kikosi cha Arsenal usiku huu: Szczesny 6, Sagna 7, Mertesacker 7, Vermaelen 7, Gibbs 7, Ramsey 6, Arteta 7, Walcott 6, Ozil 6, Rosicky 6, Giroud 6.
Wachezaji wa akiba: Podolski, Monreal, Cazorla, Flamini, Fabianski, Bendtner, Jenkinson.
Kikosi cha Chelsea: Cech 6, Ivanovic 7, Cahill 7, Terry 7, Azpilicueta 7, Mikel 6, Lampard 7, Ramires 6, Willian 6, Hazard 7, Torres 6.
Wachezaji wa akiba: Cole, Luiz, Mata, Oscar, Schurrle, Schwarzer, Eto’o.




0 comments:
Post a Comment