Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa
Askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Mashirika na Taasisi
zisizo za Serikali pamoja na wakazi wa Temeke kabla ya kuzindua Mpango
Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto
ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi
Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP) Said Mwema. Waziri Nchimbi katika hotuba yake
alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi
zisizo za Serikali kwa kusaidia kupambana na unyanyasaji wa kijinsia
nchini. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikionyesha kitabu cha
Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na
Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha
Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wapili kushoto ni Balozi wa
Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Waziri Nchimbi katika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na
Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia
kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini. Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wasita kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi
wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali baada ya waziri huyo kuzindua
Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na
Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi
Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Watano kulia ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema. Waziri Nchimbi katika hotuba
yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na
Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia kupambana na unyanyasaji wa
kijinsia nchini. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


0 comments:
Post a Comment